Nyumbani
Sisi Ni Akina Nani Mashujaa Picha Tuzo Uongozi
Academy
Overview The Programme The Journey
Blog Join Us Mentors Sign In
English Kiswahili
Hali ya giza
Wasiliana Nasi

About Mpangomzima

Mpangomzima Academy is a Business Growth and Leadership Operating System built inside www.mpangomzima.com to make members of Mpangomzima into capable business leaders within BF SUMA.

Who we are

Our Story

Mpangomzima Academy ni mfumo wa kisasa wa mafunzo (Learning Management System) unaopatikana ndani ya www.mpangomzima.com, ulioundwa kwa lengo la kuwajenga wanachama wa Mpangomzima kuwa wafanyabiashara na viongozi wenye uwezo mkubwa ndani ya BF SUMA. Mpangomzima Finance pia inaendeleza Mpangomzima Leaders Academy, jukwaa la mentor-marketplace linalowawezesha viongozi waliohitimu kujenga profaili za umma, kuchapisha maudhui, na kupatikana na wateja watarajiwa.

Dhamira Yetu

Kuwapa wanachama wote wa Mpangomzima mfumo wa kujifunza unaowawezesha kujifunza kwa mpangilio, kujenga biashara yenye matokeo, kukuza viongozi, na kufikia ngazi ya Senior Crown Leader (SCL) ndani ya mwaka mmoja kupitia mtaala rasmi wa Mpangomzima.

Maono Yetu

Kuwa jukwaa bora zaidi barani Afrika la kujenga wafanyabiashara na viongozi wa BF SUMA kupitia mfumo wa mafunzo unaotumia teknolojia, unaopima maendeleo na unaozalisha matokeo halisi.

Ukuaji

Mfumo wa Mpangomzima Academy umeundwa kutatua changamoto za mafunzo yasiyo na mpangilio, ukosefu wa ufuatiliaji wa maendeleo, na sponsors kutokujua maendeleo ya timu zao. Kwa kuunganisha mafunzo ya 90 Days Orientation, First Twelve (180 Days) na Second Eight (90 Days), mfumo unatoa njia iliyo wazi ya kumwezesha mwanachama mpya kukua hatua kwa hatua hadi kufikia ngazi ya Senior Crown Leader (SCL) ndani ya mwaka mmoja, huku sponsors na wasimamizi wakipata mwonekano wa moja kwa moja wa maendeleo ya kila mshiriki.

Zaidi ya Mfumo wa Mafunzo

Mpangomzima Academy si mfumo wa kawaida wa kujifunza bali ni Business Growth & Leadership Operating System, unaounganisha elimu, ufuatiliaji wa biashara, maendeleo ya viongozi, tathmini za utendaji na teknolojia katika jukwaa moja.

Focus areas

What the Academy is built on

01 Elimu (Mafunzo)
02 Nidhamu
03 Ufuatiliaji
04 Matokeo
05 Ukuaji
Barua pepeinfo@mpangomzima.com
AnwaniDar es Salaam, Tanzania
Zungumza na timu yetu